Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Machi 7,2024 amekabidhi pikipiki 24 aina ya boxer zenye thamani ya milioni 72 kama vitendea kazi kwa sekta ya mifugo katika Mkoa huo.
Akiongea na Wataalam waliokuja kupokea pikipiki hizo kutoka Wilaya zote za Mkoa huo amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kwa jitihada yake kubwa katika Kuboresha Sekta mbalimbali hapa nchini ikiwemo Sekta ya mifugo ambapo kupitia wizara ya mifugo na uvuvi ametoa pikipiki hizo kwa Mkoa wa Dar es Salaam.
Aidha RC Chalamila amewataka wataalam hao kutumia pikipiki hizo vizuri,kwenda kuelimisha na kuhamasisha jamii ufugaji wa kisasa na wenye tija ambao utawezesha kujikwamua kiuchumi kuondokana na umasikini.
Vilevile ametoa taadhari ya matumizi mabaya ya vyombo hivyo kwa kuwa ni vyombo vya moto ni vema vitumike kwa uangalifu mkubwa.
Naye Katibu Tawala msaidizi uchumi na uzalishaji Mkoa Dkt Elizabeth Mshote amesema sekta ya mifugo katika Wilaya zote za Mkoa wamepatiwa pikipiki 24 kwa mgawanyo ufuatao Halmashauri ya Jiji pikipiki 5, Kinondoni 4, Temeke 5, Ubungo 5, na Kigamboni 5 hata hivyo watumishi ambao wamepata pikipiki na wana leseni ya kuendesha pikipiki ni 14 kati ya 24
Mwisho ifahamike kuwa Mkoa wa Dar es Salaam unaowafugaji wengi hususani ufugaji wa kisasa hivyo kupatikana kwa vitendea kazi hivyo kukwenda kuinua sekta hiyo muhimu kwa masilahi mapana ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa Ujumla.