WAZIRI Wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Silaa amesema kuwa Mkoa wa Dar es Salaam umekithiri kwa uvamizi wa ardhi hasa kwa baadhi ya wananchi kununua maeneo na kuyaendeleza bila kujua uhalali wa umiliki wa eneo husika wakati akizungumza na Waandishi wa habari katika ofisi ya wizara ya ardhi Dar es Salaam.
Waziri pia amesema itaanzisha Operesheni kuhakikisha uvamizi wa ardhi hasa kwa wale vinara wa matapeli papa wa ardhi wakiwemo 7 ambao tayari wamepatikana huku bawili kati yao wakiwa wameshaanza kushughulikiwa.
‘Hali ya uvamizi wa ardhi kwa Mkoa wa Dar es Salaam imekithiri kwa kiasi kikubwa, watu wana hati za umiliki wa maeneo lakini hawawezi kuendeleza maeneo hayo…Wanatokea wajanja wanauza eneo hilo kwa mtu mwingine ambaye haulizi uhalali wa eneo hilo na sisi tumepewa maelekezo na rais Samia Suluhu kuhakikisha ddhuluma kwenye suala la ardhi linakwisha’