Klabu ya Serie A ya Lazio imekanusha ripoti kwamba kocha Maurizio Sarri ataondoka mwishoni mwa msimu huu.
Meneja huyo wa zamani wa Chelsea, Napoli na Juventus ana mkataba hadi Juni 2025.
Lakini huku Lazio wakiwa wameshinda mchezo mmoja tu kati ya mitano iliyopita na kwa sasa wakiwa katika nafasi ya tisa kwenye Serie A, kulikuwa na uvumi kwamba klabu hiyo ilikuwa inatafuta meneja mpya.
Taarifa ya klabu ilisema: “Kufuatia habari zilizoonekana kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuhusu madai ya tathmini zinazoendelea kwenye mwongozo wa kiufundi, S.S. Lazio inathibitisha, ikiwa ni lazima, imani yake kamili kwa kocha Maurizio Sarri, ikibainisha kuwa kocha mwenyewe ana mkataba unaomalizika 2025. . Kwa hivyo, uvumi wote ambao ungeunganisha makocha wengine na S.S. Lazio hauna msingi wowote.”