Ni sehemu ya wachezaji wa Tanzania ambao wanapata nafasi ya kucheza nje ya nchi leo TFF wametangaza wachezaji watano walioombewa hati ya uhamisho wa kimataifa ITC ili wakachezea mpira nje ya Tanzania.
Miongoni mwa wachezaji hao ni pamoja na Abdulhalim Humoud kutoka Simba,Crispine Odulla (Coastal Union) pamoja na Haji Ugando (Mbagala Market FC) wameombewa ITC na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kenya (FKF) ili wakacheze Kenya kwenye klabu za Sofapaka,Bandari FC na Nakuru All Stars.
Mbali na hao TFF pia imemuombea ITC mchezaji Ismaila Diarra kutoka nchini Mali ili aweze kujiunga na timu ya Azam FC kwa sasa TFF inafanyia kazi maombi hayo na taratibu zote zitakapokamilika itatoa ITC hizo kwa wachezaji wanaokwenda nje ya Tanzania