MNEC MLAO asema mgombea Mketo ndiye Chaguo la Wananchi na Chaguo la CCM Uchaguzi mdogo Kata ya Mlanzi Kibiti.
MNEC MLAO, akiwa ndiye mgeni Rasmi kwenye Ufunguzi wa Kampeni amemnadi mgombea ndugu Athuman Ally MKETO (Fella) kwa tiketi ya CCM na Kuwasihi wananchi wa Mlanzi CCM imemleta mtoto wenu, ambaye ni mwadilifu, na mwenye kuijua vyema kata hii ya Mlanzi, Sasa Shikamaneni nae akafanye kazi ya kuleta Maendeleo hapa.
MNEC MLAO, akasisitiza Wakati ni sasa, Mchagueni Mketo akatekeleze Vyema Ilani ya CCM kwenye hii Kata, kwa Kasi zaidi, kwani ni mwenye Sifa njema na ni Kijana Mchapakazi kweli.
MNEC Mlao aliendelea Kusema, ndugu zangu Mheshimiwa Rais DKT SAMIA amefanya Kazi kubwa ya kuleta Fedha nyingi za Miradi ya Maendeleo hapa Kibiti, tunzeni miradi hiyo kwa faida ya Sasa na ya baadae.
MNEC alimuombea Kura ndugu Mketo na Wananchi Wakajibu kwa Sauti Moja kwamba ndiye chaguo lao na ndiye Chaguo la Wananchi wa Mlanzi, Watampa Kura za Kishindo ifakapo tarehe 20/03/2024.