Zaidi ya watu 300 wamepatiwa matibabu bure kwa magonjwa mbali mbali mkoa wa Kaskazini Unguja visiwani Zanzibar kwenye Kambi ya siku 5 ya matibabu inayoongozwa na Mke wa Rais wa Zanzibar mama mariam Mwinyi
Mama Mariam Mwinyi ambae amekua akiendesha kampeni ya maisha Bora lishe bora chini ya Maisha Bora Foundation (ZMBF) Imezamiria kuzunguka Zanzibar nzima na kutoa huduma ya afya ambayo haichangiwi ambayo imeanza na kudhuriwa na watoto ,watu wazima na Wazee
miongoni kati huduma zizokua zinatolewa ni pamoja na huduma ya lishe bora kwa mam na mtoto ,upimaji wa magonjwa ya moyo,matibabu ya uzazi kwa akina mama ,presha ,matatizo ya macho ,uzito uliopitiliza ,upimaji wa matatizo mbali mbali na kupewa Dawa Nk.
” Zanzibar Maisha Bora Foundation katika utekelezaji wa afua zake imekuwa ikitafuta uwiano na tunaamini kuwa Udhalilishaji na Ukatili wa kijinsia unaathiri hali za kiafya tumetumia fursa hii ya kambi ya matibabu Mkoa wa Kaskazini Unguja 2024 kuzindua rasmi kampeni ya Zanzibar “Says No More” chini ya Jumuiya ya Madola yenye maana ya “Ukatili Zanzibar Sasa Basi-Mama Mariam”