ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Simba, Ismail Rage, ameshusha pumzi na anakwenda kupumzika huku akidai kuiacha Simba na mambo matatu ya kihistoria.
Wakati akiwa amekamilisha uongozi wake kwa klabu ya soka ya Simba, Ismail Aden Rage amefafanua mambo makubwa matatu aliyoiachia klabu hiyo kabla ya kukabidhi mikoba.
Rage amesema cha kwanza kikubwa ni akaunti ya klabu yenye kitita cha Shilingi milioni 420 , pili ni Uwanja wa Bunju na tatu makubaliano yake na Benki ya Posta kuhusiana na kadi za wanachama ambazo kama uongozi mpya utakuwa makini, klabu itaingiza pesa nyingi kupitia mtindo huo.
Akikokotoa kiasi hicho cha Sh420 milioni, Rage alisema kati ya hizo zimo Sh60 milioni za mauzo ya Shomari Kapombe aliyesajiliwa na Azam FC, Sh160 milioni za kodi ya mapango ya jengo la Simba lililopo Kariakoo jijini Dar es Salaam na Sh100 milioni za wadhamini.
Akizungumza na Mwanaspoti pia Rage alionyesha hisia zake juu ya kero alizokuwa anakutana nazo alipokuwa madarakani, alisema: “Kuongoza klabu kubwa kama Simba ni lazima ujitoe, hata hivyo vurugu kubwa za klabu ambazo zinatokea huwa zinasababishwa na njaa tu. Hivyo kumaliza muda wangu nashukuru maana nakwenda kupumzika.”
Source: Mwanaspoti
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta FB