Dayot Upamecano ameweka wazi kuwa hafikirii kuondoka Bayern Munich msimu wa joto.
Dayot Upamecano, ambaye alitazama akiwa kwenye benchi mechi ya Bayern ilipoilaza Mainz 8-1 Jumamosi, anaripotiwa kuwa mmoja wa wachezaji wa Bayern ambao hawakuwa na uhakika wa mustakabali wake.
Hata hivyo, beki huyo wa kati hana nia ya kutaka kuondoka katika klabu hiyo ya Bavaria.
“Hapana, hata kidogo,” aliambia Kicker alipoulizwa kama anafikiria kuhama majira ya kiangazi.
“Nina mkataba hadi 2026, najisikia vizuri – katika klabu na wachezaji wenzangu. Nataka kusalia hapa FC Bayern na nitaendelea kujitolea,” Upamecano aliongeza.