Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Chama Cha Mapinduzi Taifa Comred Maganya Rajabu amefanya ziara wilayani Mbogwe Mkoani Geita katika kutembelea na Kukagua Miradi inayotekelezwa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi pia amefungua rasmi Kampeni za Uchaguzi Diwani Kata ya Isebya kwa tiketi ya Chama hicho na kuwataka wananchi kufanya uchaguzi wa huru na haki.
Akizungumza na Wananchi wa kata ya Isebya Comred, Rajabu amesema lengo la Chama cha Mapinduzi ni kuleta Mabadiliko chanya katika kuelekea Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa huku akiwahasa wananchi kumchagua Gorge Masorwa Machi 20 mwaka huu .
Mbunge wa Jimbo la Mbogwe , Nikodemas Maganga amewataka kupuuza baadhi ya maneno ambayo yamekuwa yakiongelewa na wananchi kuwa hakuna kilichofanyika katika kata hiyo huku akisema Diwani aliyefariki dunia ameondoka akiwa amefanya mengi kwa wanaisebya.
“Hakuna kurudi nyuma ndugu zanguni wanaisebya nawapenda sana bila shaka hata na nyie ni mashaidi nilipoingia madarakani 2021 isebya haikuwa na zahanati kupitia Mfuko wa Jimbo nilileta mabati isebya nikiwa na Mh Diwani ambaye ni marehemu kwa sasa na Mungu amuweke mahala pema peponi Amina, ” Mbunge Maganga.
Ziara ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa ina lengo la kutembelea na kukagua Miradi mbalimbali katika Majimbo yote ya Geita kwa lengo la kuonyesha kwa watanzania yale yaliyofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.