Familia ya staa wa zamani wa Barcelona na Brazil Dani Alves imezika tetesi zinazodai kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 40 amefariki.
Uvumi kwamba Alves alijitoa uhai ndani ya jela ambako amefungwa kwa miaka minne unusu baada ya kupatikana na hatia ya ubakaji uliibuka siku ya Jumamosi jioni baada ya mwanamtandao kuchapisha kuhusu hilo.
Siku ya Jumapili, Nay Alves, kaka wa mwanasoka huyo wa zamani wa Brazil hata hivyo alitoa taarifa akiuhakikishia ulimwengu kuwa mwanasoka huyo yu hai na hajajitoa uhai kama ilivyodaiwa. Pia alichukua fursa hiyo kuwakashifu walioibua madai hayo ya kuhuzunisha
“Binadamu ni wakatili kiasi gani. Tayari alihukumiwa kwa maneno ya mwanamke aliyeingia kwenye chumba cha wanaume kufanya kile anachojua yeye tu na yeye.
Tayari ameshahukumiwa, haitoshi?” kaka wa mchezaji huyo wa zamani aliandika kwenye Instagram akisindikizwa na picha ya wawili hao wakiwa pamoja.