Mafuriko yaliyofuatwa na maporomoko ya ardhi yaliyopiga kisiwa kikubwa cha Sumatra nchini Indonesia yamesababisha vifo vya watu 26 na takriban 11 kutoweka, kulingana na ripoti mpya iliyotolewa siku ya Jumatatu, Machi 11, na idara ya huduma za dharura.
“Watu 11 wametoweka na wengine 26 wamepatikana wamefariki,” amesema Abdul Muhari, msemaji wa Shirika la Kukabiliana na Maafa katika taarifa yake. Mvua kubwa ilisababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi katika wilaya ya Pesisir Selatan, katika jimbo la Sumatra Magharibi, na kuwalazimu zaidi ya watu 75,000 kukimbilia katika makazi ya muda, linaandika shirika la habari la AFP.
Mvua kubwa iliyonyesha ilisababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi katika wilaya ya Pesisir Selatan mkoa wa Sumatra Magharibi, na kuwalazimu zaidi ya watu 75,000 kutafuta makazi katika makazi ya muda.
Katika wilaya hiyo, watu 23 wamefariki, huku sita wakiwa bado hawajulikani walipo, kulingana na Fajar Sukma, mkuu wa idara ya huduma za dharura wa eneo hilo.
Watu wengine watatu walmefariki katika hali mbaya ya hewa katika wilaya ya Padang Pariaman. “Idadi ya vifo inaweza kuongezeka zaidi,” ameonya Bw. Sukma.