Wakati Ramadhani ikiwa inaanza kwa jamii ya Waislamu duniani kote, serikali ya Uingereza inatangaza uwekezaji wa pauni milioni 117 kulinda maeneo ya ibada na vituo vya kitamaduni.
Waislamu nchini Uingereza kwa sasa wanakabiliwa na ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu.
Zaidi ya euro milioni 120 zitatengwa kwa muda wa miaka minne ili kufunga kamera za uchunguzi, uzio unaostahimili zaidi na mifumo ya kengele katika misikiti, shule za Kiislamu na maeneo ya kitamaduni.
Njia ya kulinda maeneo yanayohusiana na Uislamu na waumini kutokana na mashambulizi ya chuki dhidi ya Uislamu.
Kulingana na chama ambacho hukusanya shuhuda kutoka kwa waathiriwa, mashambulizi haya yaliongezeka mara tatu kati ya mwezi Oktoba na Februari, ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka mmoja mapema.
Shirika lisilo la kiserikali la Tell Mama inaunganisha moja kwa moja kati ya ongezeko hili la mashambulizi na vita huko Gaza.
Matukio haya yanahusisha zaidi matusi kwenye mitandao ya kijamii, lakini pia vitisho vinavyorushwa misikitini na matusi mitaani. Wanawake wanawakilisha thuluthi mbili ya waathiriwa.