Joao Cancelo amethibitisha kuwa anatumai kuona uhamisho wake wa mkopo kutoka Manchester City kwenda Barcelona unakuwa wa kudumu msimu huu wa joto.
Beki huyo wa pembeni wa Ureno alijikuta akikosa kibali chini ya Pep Guardiola msimu uliopita kabla ya kufunga uhamisho wa mkopo kwenda kwa wababe hao wa Catalan mnamo Septemba kufuatia kipindi cha kwanza akiwa na Bayern Munich.
Katika mahojiano na jarida la Kiitaliano Gazzetta dello Sport, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 alisema: “Kwa mkopo kutoka Man City? Sijui mustakabali wangu bado lakini ningependa kusalia Barcelona.
“Nilikua na Ronaldinho kama idol wangu, najivunia kuvaa shati la Barca.”