Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya kuzuiya rushwa na uhujumu uchumi zanzibar (ZAECA) Zanzibar Ali Abdallah Ali ,amesema mamlaka iyo iko njiani kurudisha fedha zilizotokana uhalifu ikiweko rushwa na uhujumu uchumi ambapo mamlaka iyo itapora mali zote endapo utabainika kwa maswala ya uhujumu uchumi.
Ameyasema hayo wakati wa mafunzo wa watendaji wa ZAECA na wafanyakazi wa Tasisi mbali mbali za serikali Baada ya kupatiwa mafunzo hayo na ACFE Inayojishulishw na maswala ya rushwa na uhujumu uchumi Tanzania.
” Tupo katika hatu ya kurejesha fedha ambazo zimetokana na madhalia ya uhalifu ikiwemo makosa ya rushwa,uhujumu uchumi ,ubadhirifu utakatishaji wa fedha haramu na makosa mengine ,tunazo mali zao mbali mbali magari ,nyumba ,viwanja tunavidhibiti andapo kesi tumeshinda mahakamani tunaiyomba mahakama kuchukua mali zote zilizotokana na uhalifu na kurudi serikalini—Ali Abdallah Mkurugenzi ZAECA