Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa ameendelea na kliniki ya Ardhi kwa ajili ya kusikiliza migogoro ya Ardhi ndani ya mkoa wa Mwanza ambapo amekuwa akifika kila siku saa 1:00 Asubuhi na kuanza kusikiliza wananchi katika viwanja vya Nyamagana jambo ambalo limeshangaza wengi kwa kiongozi huyo kufika mapema kila siku asubuhi.