Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa taasisi za kiserikali na Sekta binafsi kufanya jitihada za kuhakikisha Wanawake wanapata nafasi na kusikika kwe nye maamuzi mbalimbali nchini.
Rais Samia amesema hayo leo kwenye Mkutano wa Wanawake walio katika Sekta ya fedha uliofanyika ukumbi wa hoteli ya Kwanza iliyopo Kizimkazi.
Aidha, Rais Samia amesema ushiriki wa Wanawake Kwenye ngazi za maamuzi ni suala jumuishi na endelevu hivyo halipaswi kuchukuliwa kama la kimapinduzi au la Serikali pekee.
Rais Samia amebainisha kuwa lengo ni kuhakikisha masuala yanayowahusu Wanawake ambayo wafanya maamuzi wengine wanaweza wasiwe na uelewe nayo yanapata nafasi kwenye meza ya maamuzi.
Hali kadhalika , Rais Samia amesema pamoja na kuongeza ushiriki wa Wanawake kwenye ngazi za maamuzi lazima pia kuweka nguvu kubwa katika kuwainua Wanawake kiuchumi.
Kwa Upande mwingine, Rais Samia amewatakia Wanawake kujipanga na kufikia malengo yao kwa Vitendo.