Katika kuhakikisha vifo vya Mama na Mtoto vinapungua, Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imesema Serikali inatoa huduma bure, huku miongoni mwa sababu za vifo ni ukosefu wa vifaa tiba.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Katibu Tawala wa Kinondoni, Stella Msofe amesema wapo wadau ambao sio welevu ambao wakitoa msaada wanataka kupitisha magendo jambo ambalo sio sahihi.
“Ndio maana kuna wadau tunawaita welevu na kuna wale ambao sio welevu wao wakitoa Kitanda wanataka kupitisha na magendo,”
DAS Msofe amesema kuwa Rais wa Tanzania, Dr.Samia Suluhu Hassan anahakikisha huduma za Mama na Mtoto zinatolewa bure ikiwemo kuanzishwa kwa mifumo mbalimbali.
“Rais wetu anapambana na ndio maana kuna huduma ambazo hata mataifa mengine yanajifunza kwetu, tuwashukuru wadau wetu kwa kuendelea kutusaidia hususan kwenye upande wa vifaa,”
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa GADA, Charles ambao wametoa msaada wa vifaa tiba amesema wao kama wadau wataendelea kuunga mkono juhudu za serikali.