Kiongozi wa upinzani mwenye ushawishi mkubwa nchini Senegal Ousamne Sonko na mgombea wa urais anayeunga mkono katika uchaguzi wa Machi 24, Bassirou Diomaye Faye, waliachiwa huru kutoka jela Alhamisi, televisheni ya serikali ya Senegal RTS ilisema kwenye tovuti yake.
Ousmane Sonko akiwa na mgombea mwenza Basirou Diomaye Faye waliachiliwa siku 10 kabla ya uchaguzi wa rais.
Waliondoka katika gereza la Cap Manuel kwa gari lililokuwa na vioo vya giza muda mfupi kabla ya saa sita usiku.
Kuachiliwa kwao kulikuwa kunatarajiwa kufuatia sheria ya msamaha iliyopitishwa na bunge tarehe 6 Machi, huku viongozi wakijaribu kupunguza mvutano baada ya mpango wao wa kuahirisha uchaguzi kwa miezi 10 kukwama.
RTS haikutoa maelezo zaidi, na haikufahamika mara moja wawili hao walielekea wapi baada ya kuachiliwa.
Maelfu ya wafuasi walikusanyika barabarani anakoishi Sonko mjini Dakar, wakiimba jina lake na kucheza huku wakishikilia mabango yenye picha yake.
Ousmane Sonko alikamatwa mwishoni mwa Julai baada ya shutuma za wito wa uasi, miongoni mwa mengine. Waliachiliwa jana Alhamisi jioni kufuatia kupitishwa kwa wabungewa Senegal kwa sheria ya msamaha juu ya uhalifu uliofanywa wakati wa maandamano ambayo yalifanyika kati ya Februari 2021 na 2024.