Chama cha ACT Wazalendo kimeweka bayana dhamira yao ya kuonana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Ali Mwinyi kujadili mustakabali wa Serikali ya Umoja Kitaifa na utekelezaji wa kile wanachodai kuwa hoja Tatu za makubaliano baina ya Dk. Mwinyi na Maalim Seif Sharif Hamadi.
Hayo yameibuka kufuatia Halmashauri kuu ya Chama cha ACT Wazalendo kutangaza hadharani dhamira yake ya kujitoa katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) kwa kile wanachodai kutotekelezwa kwa hoja Tatu ikiwemo fidia kwa waliyopata madhara katika Uchaguzi Mkuu Mkuu mwaka 2020, kuundwa Tume ya Kijaji kuchunguza uvunjifu wa haki za binadamu kwenye Uchaguzi Mkuu 2020 na mageuzi katika mfumo wa uchaguzi.