Star Wema Sepetu leo hii amekutana na waandishi wa Habari kuzungumza nao ambapo kubwa alilowaitia ni kuwatangazia ubalozi wa moja ya kampuni ya Beti ambao kapatiwa
Baada ya kutambulishwa Wema alifunguka kuhusu deal hilo na pale waandishi walipotaka aongelee yale yanayomuhusu kuhusu yeye na mpenzi wake Whozu kudaiwa kugombana alikwepa na kuondoka eneo la tukio
Hata hivyo waandishi hawakumuacha walimfuata na kumuuliza kama yupo Sawa, kwani alipost kuonesha hayuko sawa baada ya taarifa kusambaa mtandaoni kuwa kapigwa na mpenzi wake Whozu
“Mimi niko salama kabisa, nataka kuwajukusha niko sawa kabisa, naendelea kupona, niko sawa kabisa” Wema Sepetu