Obadia Mwalyego mkazi wa Itulahumba wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe anatuhumiwa kuwabaka watoto wake wawili wa kufikia (kambo) kwa nyakati tofauti akiwemo mwenye umri wa miaka 12 anayesoma darasa la tano na mwingine mwenye umri wa miaka 17 anayesoma kidato cha nne wilayani humo.
Akizungumza mbele ya viongozi wa Jumuiya ya wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) mkoa wa Njombe namna alivyofanyiwa ukatili huo mtoto huyo mwenye umri wa miaka 12 amesema,baba yake alimgongea dirishani usiku wa saa tano ili amfungulie mlango na kumshika kisha kumpeleka kwenye pagale ambalo limepandwa mboga mboga na kumfanyia ukatili huo huku akimtishia kumuua endapo atapiga kelele au atamwambia mamake.
Stella Ndondole ni mlezi wa mtoto huyo ambaye ni mdogo wake kiukoo amesema siku ya tukio alitoka nje majira ya usiku ili kutizama watoto kwa kuwa ni kawaida yake kuangalia watoto lakini alipofika kwenye chumba cha watoto hakuweza kumuona lakini wakati akiendelea kumtafuta alimkuta mume wake akiwa amemlali kwenye jumba bovu na kulazimika kuita mgambo ili waweze kusaidia kumkamata.
“Nimeingia tu kwenye pagale nikaona mme wangu amelala na huyu mtoto alivyoniona akaamka haraka akapiga simu ikadondoka chini akanikaba akauliza uanedna wapi mimi nikasema nilikuwa natoka tu nje yani sikuonyesha dalili ya kuwa nimeona kitu kibaya kwasababu ningesema nimeona kitu kibaya lazima angenidhuru kwasababu ni mkali”amesema Stella Ndondole
Hata hivyo amesema tukio hilo ni la pili kufanyiwa mtoto huyo huku akitishiwa na baba yake mlezi ambaye hana tatizo la akili licha ya kutumia pombe ambapo pia akiwa amefanya kitendo hicho cha ubakaji kwa mtoto mwingine wa sekondari.
Kufuatia kuongezeka kwa vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani humo,mwenyekiti wa UWT Skolastika Kevela amelazimika kuunda timu ya pamoja yenye wanasheria na maofisa ustawi wa jamii kwaajili ya kutoa msaada wa kisheria na haki za waathiriwa wa vitendo hivyo ili kukabiliana na vitendo hivyo ambapo tayari kesi dhidi ya mtuhumiwa Obadia Mwalyego imekwishafikishwa Mahakamani kutokana na jitihada za serikali pamoja na jeshi la Polisi mkoani humo.