Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo amewataka wazabuni wanaopata tenda za Serikali kwenye eneo la ujenzi kutumia vifaa vinavyozalishwa ndani ya nchi ili kuokoa fedha za kigeni.
Prof. Mkumbo ametoa wito huo leo, Machi 14, Mkuranga, Pwani alipofanya ziara ya kujionea maendeleo ya wawekezaji wa ndani wa viwanda vya kuzalisha Nondo, Misumali, kofia za misumari na Mabati ambao ni kampuni ya Viwanda ya Lodhia.
Ziara hiyo imehurudhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Bi. Khadija Nassir, Mkurugenzi wa Kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na baadhi ya watumishi kutoka TIC.