Wakati hadha ya maji ikiwa inaendelea kujitokeza katika baadhi ya maeneo nchini, Wanafunzi wa Chuo cha Maji jijini Dar es Salaam wameiomba Serikali iwatumia watalaamu wasomi waliopo katika vyuo hivyo.
Akizungumza katika mkutano wa miaka 50 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho, Mwenyekiti wa UVCCM tawi la Chuo cha Maji, Alfakisadi Shilunga amesema;
“Tunapozungumzia maendeleo katika chuo cha Maji moja kwa moja tunamzunguzia Rais Dr.Sami Suluhu Hassan kwa sababu miaka iliyopita chuo chetu kilikuwa na miundombinu mibovu na programu chache lakiji hadi imeidhishwa fedha Shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya ukarabati wa vitu mbalimbali ikiwemo Library ambapo pia aliidhinisha Shilingi Bilioni 5.9 kwa ajili ya upanuzi wa madarasa,”
Kwa upande wake Rais wa Serikali ya Mapinduzi katika chuo hicho, Said Waziri Mohammed amesema..”Vijana tunatakiwa kitoa taarifa hasa tunapoona sehemu kuna mvujo kwa mamlaka husika ambapo watafika na kuzuia kwani maji yakipotea ni hasara kwa taifa”
“Hivyo vijana wa chuo cha maji tunashiriki katika kudhibiti upotevu wa maji, hivyo mamlaka za maji zote nchini hapa wawatumie wanafunzi wa chuo cha maji ambapo Wizara iwachukue wanafunzi kwa kuwapa ajira hata kwa mwaka mmoja ili wasaidie kudhiti maji,”