Wananchi wametakiwa kuacha tabia ya kutupa taka ngumu katika mito na vyanzo vya maji Ili kuepuka uharibifu ambao unasababisha mito kujaa michanga na mifereji kuzipa.
Akizungunza wakati wa zoezi la ufanyaji usafi katika mito kikundi Kaimu Mkurugenzi Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu Mhandisi Pascal Joseph amesema katika mito ambayo inapita kwenye makazi ya watu kumekua na tabia utupaji taka hovyo na kusabisha uchafuzi wa mazingira.
Mhandisi Pascal amesema katika kuadhimishi wiki ya maji ambayo inaanza kuadhimisha Machi 16 na kilele kufikia Machi 22 ambapo wameanza kufanya usafi mto kikundi ,mitaro pamoja maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Morogoro.
Kwa Upande wake Mkuu wa Maabara ubora wa maji Mkoa Morogoro Sophia Patrick amesema uchafuzi wa Mazingira unachagia gharama za usafishaji maji na gharama bili za ankara kupanda.
Amesema suala la utunzaji vyanzo vya maji,mitaro na mazingira kwa ujumla ni jukumu la kila mtu hivyo kwa yeyote atakayekamatwa hatua Kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake .
Akizungunza katika zoezi Hilo la usafi mmoja wa Wakazi wa Morogoro Abukabari Mwilima maarufu kama Mr Sounds amewashukuru Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu kwa kuwashirikisha wananchi katika zoezi hilo.
Mr Sounds amesema atakua balozi kwa wananchi katika kuhamasisha utunzaji vyanzo vya maji,mitaro pamoja mazingira kwa ujumla
Mwisho.