Mtoto wa miaka 16 Mkazi wa Tandala Wilaya ya Makete Mkoani Njombe amenusurika kifo baada kutolewa ujauzito na Dada yake aliyeingiwa tamaa ya fedha Tsh. laki tano aliyopewa na Franko Lususu (27) aliyempa mimba Mtoto huyo wakati akiwa anafanya kazi ya mgahawani baada ya kuishia darasa la saba kijijini hapo.
Mbele ya Viongozi wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Njombe walipofika kwa ajili ya kueleza ukatili waliofanyiwa ili waweze kusaidiwa, Mtoto huyo amesema alienda dukani kwa Franko ndipo akashikwa mkono na kuingizwa store alikotolewa nguo zake kisha kushiriki naye tendo la ndoa na kumsababishia kupata ujauzito.
“Akampa Dada yangu laki tano tukaenda kwa Daktari akanunua dawa za elfu 80 vidonge vinne na kuniweka kwenye ulimi wakiniambia nisinywe maji na kurudi nyumbani lakini muda ulivyoenda damu zilikuwa bado zinatoka akamwita Daktari nyumbani usiku tukaingia chumbani kwakwe na kulala kitandani akaniingiza mkono mpaka tumboni akawa anavuta huku ninalia wakafungulia kabisa na muziki, niliendelea kuumwa na kubadilika kuwa mweupe nikaenda kwa shangazi huku nalia akaniuliza nini nikamwambia Dada amenitoa mimba akasema mbona unanuka umeoza ndio tukaenda chooni akaniminya akakuta yanatoka mafinyo meupe”
Tula Mahenge ni Ndugu wa Mtoto huyo ambapo amesema kutokana na jambo hilo walimfikisha Mtoto huyo Hospitali huku Watuhumiwa wakifikishwa Polisi na kukaa kwa siku chache kisha kupewa dhamana ambapo wameendelea kuzunguka Kituo cha Polisi na Mahakamani bila mafanikio mpaka walipoambiwa mashtaka yao hayajafikishwa Mahakamani kwakuwa Hakimu yupo likizo na sasa imeshapita miezi mitatu bila kuelezwa chochote tangu Mwezi December 2023 walipopewa maelezo hayo.
@AyoTV_ imeongea na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Mahamoud Banga ambaye amethibitisha kuripotiwa kwa tukio hilo la utoaji wa mimba katika kituo cha Polisi Tandala ambapo upelelezi wa shauri hilo umekamilika na muda wowote Watuhumiwa watafikishwa Mahakamani huku Viongozi wa UWT wakiahidi kushirikiana na Mawakili pamoja na Maafisa Ustawi ili haki itendeke.