Watu zaidi ya 15,000 wameshiriki katika mbio za haki za wanawake za kilomita tano zilizofanyika jana Jumapili huko Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia.
Mbio hizo zilifanyika chini ya kaulimbiu “Kukuza Uwekezaji kwa Wanawake: Kuharakisha Maendeleo,” na ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake, ambazo zilionyesha mchango wa wanawake wa Ethiopia kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini humo.
Waandaji wa mbio hizo wamesema, kutokana na kuenea kwa migogoro, changamoto zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi na ongezeko la mgawanyiko katika jamii, haki za wanawake zinazidi kutishiwa, na kusisitiza kuwa ni muhimu sana kulinda haki za wanawake hivi sasa kuliko wakati mwingine wa hapo awali.