Putin amewashukuru wananchi kwa kujitokeza kupiga kura, akisema ushindi wake utaiwezesha nchi hiyo kustawi.
Ameapa kuimarisha jeshi la Urusi na kutanguliza kile alichokiita “operesheni maalum ya kijeshi” ya Urusi nchini Ukraine.
Putin amesema ushindi wake unaonyesha Warusi wameungana na hatatishika
Alichukua fursa hiyo kukosoa maandamano ya ‘Mchana dhidi ya Putin’, yaliyoandaliwa na mjane wa marehemu Alexei Navalny – Yulia Navalnaya – ambayo yalifanyika katika miji kadhaa ya Urusi na vituo vya kupigia kura vya kigeni.
Putin amewaambia waandishi wa habari kwamba alikubali makubaliano ya kubadilishana ili kumwachilia huru Navalny kabla ya kiongozi huyo wa upinzani kufariki katika gereza la Arctic.
Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa kiongozi wa Kremlin kutamka jina la Navalny hadharani kwa miaka