Wanawake wilaya ya Iringa wameaswa kutumia fursa mbalimbali zinazopatikana katika jamii na kujishughulisha kufanya kazi ndogondogo za ujasiriamali ,ili kupambana na matukio ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia katika ngazi ya familia.
Hayo yamezungumzwa na mkaguzi wa polisi mkuu wa dawati la jinsia na watoto mkoani Iringa ,Elizabeth Swai alipokuwa akitoa elimu ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia,
“Kina mama waleeni watoto wenu katika maadii mazuri msiende na watoto wenu vilabuni”.Alisistiza Swai.
Steven Mhapa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Iringa ndiye alikuwa mgeni rasmi Katika maadhimisho ya siku ya wanawake hayo ambae alimuwakilisha mkuu wa wilaya ya Iringa amewaasa wanawake kutumia majukwaa mbalimbali katika kukumbushana majukumu yao kama wanawake na kutmbua majukumu yao kama wanawake.
“Ili nyumba iwe vizuri ni lazima mwanamke asimame imara, asilimia 75 ya mafanikio kuwepo katika familia zetu yanachangiwa na uwepo wa mwanamke”. Alisema Mhapa.
Kwa upande wao wanawake wa wilaya ya Iringa kupitia risala yao kwa mgeni rasmi katika maadhimidhimisho hayo, wameipongeza serikali ya wilaya na mkoa kwa kuwawezesha kupatiwa mafunzo mbalimbali ya kijasiriamali na mafunzo ya namna ya kupambana na matukio ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia.