Harry Kane alikuwa na wikendi chungu baada ya kuvunja rekodi nyingine ya ufungaji mabao akiwa na Bayern Munich kabla ya kuumia kuelekea mwisho wa ushindi wao wa 5-2 dhidi ya SV Darmstadt.
Nahodha huyo wa Uingereza alitengeza bao la kusawazisha la Jamal Musiala baada ya Bayern kwenda mbele kwa bao 1-0 na kisha kufunga bao kwa kichwa na kuwafanya kuwa mbele kwa mabao 2-1 mwanzoni mwa kipindi cha pili.
Lilikuwa bao la 31 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 katika Bundesliga msimu huu na alihakikisha kwamba alivuka rekodi ya muda mrefu ya Uwe Seeler ya kufunga mabao mengi zaidi katika msimu wao wa kwanza wa shindano hilo, iliyowekwa nyuma mnamo 1963-64.
Kane alipata matibabu uwanjani kutoka kwa timu ya madaktari ya Bayern uwanjani kabla ya kuondoka katika kile ambacho mashabiki wa England watatumaini kuwa ni ishara chanya kabla ya michuano ya Uropa msimu huu.
Ninaelewa kuwa Kane anatakiwa kuripoti kwa majukumu ya kimataifa na wachezaji wengine wa kikosi siku ya Jumanne ambapo atafanyiwa tathmini zaidi.
Three Lions watamenyana na Brazil Jumamosi Machi 23 na kisha Ubelgiji Jumanne Machi 26 katika michezo yao ya mwisho ya maandalizi kabla ya Euro kuanza.