Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Rebbeca Nsemwa amewataka wahudumu wa Mabasi ya masafa marefu na mjini kuwa na lugha nzuri Kwa abiria na kjtambua kuwa hiyo ndiyo Kazi Yao inayowaingizia kipato
Akifungua mafunzo ya wahudumu hao yaliyofanyika Mjini Morogoro yaliyoandaliwa na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kushirikiana na Mamlaka ya Uthibiti usafiri ardhini (LATRA) ambapo DC Nsemwa amesema kumekua na tabia baadhi ya wahudumu kugombana na abiria na kuleta sintofahamu katika safari
Anasema mafunzo hayo ni hatua nzuri itakayoongeza weredi wa kazi kwa wahudumu hao kwani watakuwa wanafanya Kazi vizuri pia wanatamburika rasmi na serikali.
Serikali kupitia chuo cha taifa cha usafirishaji(NIT) kwa kushirikiana na Mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini (LATRA) Wameanza kuwatambua rasmi watoa huduma wa mabasi ya masafa marefu na mijini kwa kuwapatia mafunzo yatakayowasaidia kuongeza weledi katika utendaji kazi ndani ya sekta hiyo ya usafirishaji nchini.
Kwa upande wake naibu mkuu wa chuo anayeshughurikia utalawa na fedha kutoka chuo cha taifa cha usafirishaji(NIT) Zainabu Mshana amsema mafunzo hayo yataongeza hali ya usalama wa abiria na mali zao na kwamba yatakua ni endelevu huku afisa mfawidhi wa mamlaka ya udhiti usafiri ardhini(LATRA) Andrew Mlacha akibainisha kuwa kupitia mafunzo hayo watapata takwimu sahihi zitakazowawezesha kuwatambua rasmi watoaji huduma katika mabasi ya masafa marefu na mijini.
Nao baadhi ya washiriki wameishukuru serikali kwa hatuo hiyo muhimu ya kuwatambua rasmi kupitia mafunzo hayo ambayo ni msaada mkubwa kwao kutokana na aina ya kazi wanayoifanya kukabiriwa na changamoto mbalimbali.
Mafunzo hayo tayari yametolewa katika kanda tatu nchini na kwasasa yanatolewa katika kanda ya Morogoro ambapo jumla ya washiriki 73 wamejitokeza kupata mafunzo hayo yaliyochini ya ufadhiri wa benki ya dunia.