Maafisa wa Marekani walisafiri hadi Niger wiki iliyopita ili kuelezea wasiwasi wao kuhusu uwezekano wa nchi hiyo kuendeleza uhusiano na Urusi na Iran kabla ya serikali kuu ya nchi hiyo kufutilia mbali makubaliano ya kuwasimamia takriban wanajeshi 1,000 wa Marekani huko, Pentagon ilisema Jumatatu.
Pentagon iliongeza kuwa ilikuwa ikitafuta ufafanuzi kuhusu njia iliyo mbeleni. Niger ilisema siku ya Jumamosi kuwa imebatilisha “mara moja” makubaliano yake ya kijeshi na Marekani ambayo yaliruhusu wafanyakazi wa Pentagon kufanya kazi katika ardhi yake.
Msemaji wa Pentagon Sabrina Singh alisema serikali ya Marekani ilikuwa na mazungumzo “ya moja kwa moja na ya wazi” nchini Niger kabla ya tangazo la serikali ya kijeshi, na inaendelea kuwasiliana na baraza tawala la kijeshi la Niger linalojulikana kama CNSP.
“Ujumbe wa Marekani ulikuwepo ili kuibua wasiwasi kadhaa …. Tulikuwa na wasiwasi (kuhusu) njia ambayo Niger iko. Na kwa hivyo haya yalikuwa mazungumzo ya moja kwa moja na ya wazi, kuwa na wale ana kwa ana, kuzungumza juu ya wasiwasi wetu na. pia kusikia yao,” Singh alisema.