Meneja wa Mradi wa KAGIS Mkoa wa Geita Eliud Mtalemwa pamoja na wasimamizi wa mradi kutoka Canada wamesema kupitia Michezo ambayo imekuwa ikianzishwa katika kupinga vitendo vya kikatili kwa watoto mashuleni vimepungua kwa kiasi chake kutokana na kampeni ambazo zimekuwa zikifanywa na Serikali kwa kushirikiana na shirika hilo.
Akizungumza Mara baada ya kumalizika kwa Michuano ya KAGIS CUP kwa wanawake iliyotamatika leo kwa mikwaju ya penati Meneja Mradi Eliud Mtalemwa amesema ili kutokomeza vitendo hivyo kuna haja ya kuwekeza zaidi katika sekta ya elimu kupitia michezo hasa kwa Mtoto wa kike.
“Lakini sio tuu habari ya michezo tunaamini kwamba kupitia mchezo huu tunaamini kwamba kupitia mchezo huu jamii imeweza kuhasika kuhusiana na masuala ya kupinga vitendo vya kikatili lakini kuona haja ya kuwekeza kwenye elimu , ” Meneja Mradi KAGS Mtalemwa.
Hilida Mashauri ni Msimamizi wa Masuala ya Jinsia katika Mradi wa KAGS amesema wao kama shirika wamekuwa wakitambua umhimu wa michezo kwa msichana kuwa kila mtoto ana haki ya kucheza na kila msichana ana haki ya kushiriki katika michezo mbalimbali kwahiyo kupitia michezo ambayo imekuwa ikiandaliwa imesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza vitendo vya kikatili.
“Na hii yote kumuwezesha msichana kwanza aweze kupata nafasi ya yeye kushiriki kwenye michezo kama ambavyo kijana anaweza akashiriki lakini pia wakati wa hii michezo tunakuwa tunatoa tunasema ujumbe malimbali kwa kuwafikia watoto wa kike, ” Msimamizi wa Masuala ya Jinsia Mradi wa KAGS.
Selemani Maushi ni Afisa Mtendaji kata ya Katoro amesema uwepo wa michezo hiyo umesaidia kupunguza vitendo vya kikatili kwa mtoto wa kike kutikana na pia na elimu ambayo imekuwa ikitolewa na Jeshi la Polisi kupitia Polisi kata ambao wapo katika maeneo ambayo miradi hii imepita.