Benki ya biashara ya Ethiopia inapitia changamoto kubwa kurejesha mamilioni ya dola baada ya hitilafu iliyotokea mwishoni mwa wiki iliyopita, kitendo ambacho kiliruhusu wateja kutoa fedha bila kikomo, kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya nchini humo.
Zaidi ya dola milioni 40 ziliripotiwa kutolewa kutoka Benki ya Biashara ya Ethiopia inayomilikiwa na serikali huku pesa zengine zikiripotiwa kuhamishiwa kwa benki zingine, kwani wateja waligundua wanaweza kutoa zaidi ya pesa walizokuwa nazo kwenye akaunti zao. Shughuli za fesha zilisitishwa masaa kadhaa baadae.
Rais wa benki hiyo Abie Sano alifunguka katika mkutano na waandishi wa habari kwamba sehemu kubwa ya fedha hizo zilitolewa na wanafunzi huku BBC ikiripoti kuwa mistari mirefu iliundwa kwenye ATM za vyuo vikuu mbalimbali nchini humo. Vyuo vikuu kadhaa vimewataka wanafunzi kurudisha pesa ambazo sio zao huku ikiripotiwa kuwa mtu yeyote ambaye atarejesha pesa hizo hatashtakiwa kwa makosa ya jinai.
Katika post kwenye mtandao wa X, Benki ya CBE ilithibitisha kukatizwa kwa huduma hiyo lakini ilikanusha kuwa changamot zima ilikuwa matokeo ya shambulio la mtandao. Iliongeza kuwa huduma zake za ATM sasa zinafanya kazi kikamilifu.
Benki kuu ya Ethiopia, ambayo inasimamia sekta yake ya kifedha, ilisema katika taarifa kwamba changamoto hio ilitokana na ukaguzi wa usalama wa mfumo wa fedha na “sio tukio ambalo linahatarisha benki, wateja wake na mfumo mzima wa kifedha.