Umoja wa Mataifa ulionya Jumanne kwamba vikwazo vikali vya Israeli juu ya misaada katika Gaza iliyoharibiwa na vita na uhasama unaoendelea vinaweza kumaanisha kuwa inatumia njaa kama “silaha ya vita”.
Msemaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu Jeremy amesema kiwango cha kuendelea kwa vikwazo vya Israel dhidi ya kuingia kwa misaada katika Gaza, pamoja na namna inavyoendelea kufanya uhasama vinaweza kuwa ni kutumia njaa kama njia ya vita, jambo ambalo ni uhalifu wa kivita.
Laurence aliwaambia waandishi wa habari mjini Geneva, akiongeza kuwa uamuzi wa mwisho wa kama “njaa inatumika kama silaha ya vita” utaamuliwa na mahakama ya sheria.