Jeshi la polisi nchini Brazil limesema kuwa linawashikilia watu 11 ambao wametengeza kundi linalojihusisha na uuzaji wa tiketi za kombe la dunia kinyume cha sheria.
Mtandao huo unadaiwa kuwa limejipatia fedha kinyume cha sheria kwa kuuza tiketi na tayari wamefanya uhalifu huo katika viwanja vinne vya kombe la dunia.
Baadhi ya tiketi hizo zilikuwa zimetengwa kwa ajili ya wadhamini wakati nyingine zikiwa zimewekwa kwa ajili ya maafisa wa timu ya Brazil.
Polisi wanaamini kuwa baadhi ya tiketi zimeuzwa kwa watalii wa kigeni.