Ushindani wa teknolojia kati ya Marekani na China uliibuka tena baada ya jaribio la zamani la kupiga marufuku mtandao wa kijamii wa TikTok, unaomilikiwa na kampuni ya Kichina ya ByteDance, kwa misingi ya usalama wa taifa.
Marekani inaona jukwaa hilo kuwa tishio kutokana na masuala ya usalama na uhusiano unaodaiwa kuwa wa kampuni hiyo na serikali ya China.
Rais wa Marekani Joe Biden amesema atatia saini mswada huo iwapo Bunge la Congress litaamua kuzuia ufikiaji wa TikTok, na Baraza la Wawakilishi likaupitisha, na hivyo kufungua njia ya kupiga marufuku TikTok kote nchini kwa sababu “inaleta shida ya usalama wa kitaifa.”
Huko Beijing, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Wang Wanbin aliishutumu Marekani kwa kutumia suala la usalama wa taifa kutumia mamlaka ya serikali kukandamiza TikTok, licha ya kukosekana kwa ushahidi kwamba usalama wake wa taifa unatishiwa.
Kesi ya TikTok imeonyesha kwa mara nyingine tena kwamba Marekani inasisitiza sheria na utaratibu ambao unanufaisha Washington pekee, aliongeza.
Mkurugenzi Mtendaji wa TikTok Shou Zi Chew alisema katika taarifa yake ya video kwamba kampuni hiyo itafanya kila linalowezekana kulinda programu hiyo, akidai kuwa kuipiga marufuku kutahatarisha kazi za Wamarekani 300,000.