Benki ya Biashara ya Ethiopia inaendelea kupambana kurejesha mamilioni ya dola baada ya hitilafu iliyotokea mwishoni mwa wiki iliyopita, kitendo ambacho kiliruhusu Wateja kutoa fedha bila kikomo kwenye benki hiyo.
Zaidi ya dola milioni 40 (zaidi ya Tsh.bilioni 102) ziliripotiwa kutolewa kutoka Benki ya Biashara ya Ethiopia inayomilikiwa na Serikali huku pesa nyingine zikiripotiwa kuhamishiwa kwenye benki nyingine baada ya Wateja kugundua kuwa wanaweza kutoa zaidi ya pesa walizokuwa nazo kwenye akaunti zao na kupelekea shughuli za fedha kusitishwa masaa kadhaa baadaye.
Rais wa Benki hiyo Abie Sano amesema sehemu kubwa ya fedha hizo zilitolewa na Wanafunzi ambapo foleni ndefu iliundwa kwenye ATM za Vyuo Vikuu mbalimbali Nchini humo.
Vyuo Vikuu kadhaa vimewataka Wanafunzi kurudisha pesa ambazo sio zao huku ikiripotiwa kuwa Mtu yeyote ambaye atarejesha pesa hizo hatoshtakiwa kwa makosa ya jinai.
Benki Kuu ya Ethiopia, ambayo inasimamia Sekta yake ya kifedha imesema changamoto hiyo ilitokana na ukaguzi wa usalama wa mfumo wa fedha na sio tukio ambalo linahatarisha benki, Wateja wake na mfumo mzima wa kifedha.
#MillardAyoUPDATES