Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro kuelekea michezo ya robo fainali ya CAF Champions League kati ya Simba SC dhidi ya Al Ahly ya Misri na Yanga SC dhidi ya Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini amesisitiza uzalendo.
“Tunaposema sasa tunataka kusimamia uzalendo hatutanii ndio maana tunakaa na Viongozi wa Simba na Yanga ili nao wawaambie Mashabiki wao, atakayekwenda kinyume na serikali kuhusu suala la uzalendo hatuna mswalie mtume”
“Sasa kama wewe Yanga inacheza na Mamelod unataka kuvaa t-shirt ya Mamelod pale mlangoni utapita kwa passport, tuoneshe passport yako kwamba wewe ni Muafrika Kusini tutakuruhusu upite”
Simba na Yanga wataanzia nyumbani katika michezo ya robo fainali ya CAF Champions League Ijumaa Machi 29 kwa Simba kuikaribisha Al Ahly na Yanga dhidi ya Mamelod Sundowns itakuwa Machi 30 katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.