Tahadhari hii ya kuongezeka inakuja katikati ya mapambano ya muda mrefu kati ya mamlaka ya Uganda na ADF. Kundi hilo la waasi, lililoundwa katika miaka ya 1990 na watu wasioridhika na jinsi serikali inavyowatendea Waislamu, lina historia ya vurugu nchini Uganda.
Hata hivyo, baada ya kushindwa kijeshi, mabaki ya ADF walikimbia kuvuka mpaka hadi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Katika juhudi mpya za kusambaratisha ADF, Uganda na DRC zilianzisha mashambulizi ya pamoja mwaka 2021 yenye lengo la kuwaondoa wanamgambo hao kutoka katika ngome zao za Kongo.
Licha ya madai ya Rais Yoweri Museveni kufanikiwa kuwaangamiza wapiganaji wengi wa ADF, wakiwemo makamanda, kundi hilo linaendelea kufanya mashambulizi ndani ya Uganda.
Mauaji ya kikatili ya watoto wa shule magharibi mwa Uganda mwezi Juni mwaka jana na mauaji ya wanandoa waliofunga ndoa na mtembezaji watalii katika mbuga ya wanyama Oktoba mwaka jana ni ushahidi mbaya wa tishio linaloendelea la ADF.