Polisi nchini Haiti wamewauwa watu wasiopungua watatu wakati wakizuia shambulio katika benki kuu ya nchi hiyo.
“Kundi la wahalifu” lililenga Benki ya Jamhuri ya Haiti (BRH) siku ya Jumatatu, mfanyakazi aliiambia AFP, na kusababisha vifo vya watu wanne na mlinzi kujeruhiwa.
Benki ilishukuru vikosi vya usalama kwa “kulinda jamii yetu”.
Haiti imekumbwa na ghasia za wiki kadhaa baada ya magenge kuvamia magereza, kuwaachilia maelfu ya wafungwa na kumlazimisha waziri mkuu kujiuzulu.
Katika taarifa yake kwenye mtandao wa X, BRH ilisema: “Kufuatia tukio la jana karibu na tovuti [yetu] kwenye Rue Pavee, vikosi vya usalama na timu ya usalama ya benki hiyo ilifanya kazi kwa weledi na ufanisi.”
BRH iliongeza kuwa “shukrani nyingi kwa maafisa wetu na polisi wa serikali kwa umakini wao”.
Mfanyakazi huyo ambaye alizungumza na AFP kwa sharti la kutotajwa jina, alisema “watatu au wanne” wa genge hilo la wahalifu wameuawa katika shambulio hilo.