Mchekeshaji maarufu aliyejipatiia umaarufu kupitia mitandao ya kijamii Umar Lahbedi Issa maarufu kama “MZEE WA MJEGEJO” amefariki dunia jana wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mwananyama Dar es Salaam.
Akizungumza na Ayo Tv, Meneja wa Mzee wa Mjegejo, Clement Charles amesema “Mimi Mzee wa Mjegeje nilisimama kama Meneja wake nilikuwa namuomgoza kwenye kazi zake za sanaa na hata mara ya kwanza kufanya kipindi na Millard ilikuwa ni mimi namsimamia, msiba umetokea jana saa 7 alikuwa anasumbuliwa na Ini lilifeli na Figo, maziko yanafanyika leo saa 10 Keko Madukani,”.
“Mzee wa Mjegejo ameacha mtoto wa Kike mmoja ila mwanamke aliachana naye,”
Itakumbukwa kwamba Mzee wa Mjegejo aliwahi kufanyakazi na wasanii mbalimbali ikiwemo kushiriki video ya wimbo wa msanii Harmonize.