Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amepokea salamu za pole kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Wasafi Nasibu Abdul Juma almaarufu Diamond Platinumz na ujumbe wake Ikulu Mnazi Mmoja tarehe 20 Machi 2024.
Aidha Rais Dk.Mwinyi ameushukuru uongozi wa Wasafi kwa kuja kumfariji na kushiriki katika mazishi ya Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi pamoja na utayari wao kushiriki kutangaza mazuri yanayofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Halikadhalika Mkurugenzi Mkuu wa Wasafi Nassib Abdul amempongeza Rais Dk.Mwinyi kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuwaletea maendeleo Wazanzibari na kuvuka malengo ya ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 hususani katika sekta ya elimu.
Vilevile Wasafi wameahidi kuendelea kushirikiana na Rais Dk.Mwinyi na kumuunga mkono kuyatangaza mazuri yote anayotekeleza kwa wananchi wa Zanzibar, pia wamemkabidhi zawadi ya nyimbo maalum kwa ajili ya kazi nzuri alizofanya iliyotungwa na wasanii kutoka Wasafi.