Rais wa Yanga SC Hersi Said pamoja na Kamati yake ya Utendaji wamekubaliana kuwa mechi yao dhidi ya Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini siku ya Jumamosi ya March 30 2024 itakuwa bure sehemu za mzunguuko.
Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Yanga SC Ally Kamwe akieleza kuwa wameamua hivyo kwa kuzingatia kuwa mechi inachezwa usiku saa 3:00 hivyo wanawapunguzi mashabiki gharama.
Yanga wametangaza gharama zao za tiketi zitakuwa VIP A Tsh 30,000, VIP B Tsh 20,000 na VIP C Tsh 10,000