Rais Cyril Ramaphosa amethibitisha kujitolea kwa Afrika Kusini kuendelea na uhusiano na Urusi baada ya kuchaguliwa tena kwa Rais Vladimir Putin.
Ramaphosa alimpongeza Putin kwa ushindi wake wa uchaguzi uliompa muhula wa tano wa uongozi kwa miaka sita.
Putin alipata zaidi ya 87% ya kura lakini nchi za Magharibi zimepuuzilia mbali uchaguzi huo na kusema kuwa ni udanganyifu. Ameiongoza Urusi kama rais au waziri mkuu tangu Desemba 1999.
Rais wa Afrika Kusini alisema utawala wake utashirikiana na Urusi na Ukraine “katika kutafuta amani ya kudumu kati ya nchi hizo mbili jirani”, ofisi yake ilisema katika taarifa Jumatano.