Mshambulizi wa zamani wa Brazil na Manchester City Robinho amekamatwa na polisi wa shirikisho nyumbani kwake katika jiji la Santos baada ya mahakama ya Brazil kuamua anatakiwa kutumikia kifungo cha miaka tisa jela kwa kosa la ubakaji alilopatikana na hatia nchini Italia.
Mwanasoka huyo mwenye umri wa miaka 40, ambaye jina lake kamili ni Robson de Souza, aliwekwa chini ya ulinzi Alhamisi usiku baada ya mawakili wake kushindwa katika jaribio lao la kuchelewesha kuzuiliwa kwake kutokana na uhalifu wa 2013, ambao ulifanyika alipokuwa mchezaji wa AC Milan. .
Mnamo mwaka wa 2017, mahakama ya Milan ilimpata Robinho na Wabrazil wengine watano na hatia ya kumbaka mwanamke baada ya kumnywesha pombe kwenye disko.
Hukumu hiyo ilithibitishwa na mahakama ya rufaa mnamo 2020 na kuthibitishwa na mahakama kuu ya Italia mnamo 2022.