Marekani imetayarisha azimio jipya kwa ajili ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linalotetea kusitishwa kwa mapigano katika Ukanda wa Gaza, huku kukiwa na ongezeko la shinikizo la utawala wa Biden kwa Israel kupunguza mashambulizi yake.
Katika taarifa iliyotolewa jana, Nate Evans, msemaji wa ujumbe wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, alifichua kwamba Washington “imekuwa ikifanya kazi kwa dhati na wajumbe wa Baraza katika wiki kadhaa zilizopita juu ya Azimio ambalo bila shaka litaunga mkono juhudi zinazoendelea za kidiplomasia zinazolenga kupata kusitisha mapigano mara moja huko Gaza kama sehemu ya makubaliano ya mateka, ambayo yangefanya mateka waachiliwe na kusaidia kuwezesha kuongezeka kwa misaada ya kibinadamu.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken aliongeza katika ufichuzi huo wakati wa safari yake nchini Misri, akisema kuwa rasimu ya azimio hilo inataka “kusitishwa kwa mapigano mara moja kuhusiana na kuachiliwa kwa mateka”.
Akikubali kwamba kazi ngumu bado iko mbele kuhusu mpango huo, alisema: “Ninaendelea kuamini kuwa inawezekana.”
Katika wiki za hivi karibuni, mazungumzo kati ya maafisa wa pande zote yamesonga mbele na mara kwa mara yameshindwa kuleta usitishaji vita katika Ukanda wa Gaza unaozingirwa, huku kundi la Muqawama wa Palestina, Hamas, likitaka kusitishwa kwa kudumu kwa mapigano na kukomesha vita badala ya wafungwa waliosalia wa Israel.
vita, wakati Marekani na wengi ndani ya Israel wanataka kuweka kikomo makubaliano hayo kwa kusitisha kwa muda kwa wiki sita katika mashambulizi hayo.