Shirika la kutetea haki za binadamu nchini Kenya linaloungwa mkono na serikali siku ya Ijumaa lilisema maafisa wa serikali walipuuza “ripoti za kuaminika” ambazo zingeweza kuzuia vifo vya zaidi ya watu 400 wanaoshukiwa kuwa wafuasi wa madhehebu ya siku ya maangamizi.
Mirundo ya mabaki ya binadamu iligunduliwa mwezi wa Aprili mwaka jana katika msitu wa Shakahola, eneo kubwa la misitu ambalo liko bara kutoka mji wa Bahari ya Hindi wa Malindi.
Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu ya Kenya (KNCHR), chombo kinachofadhiliwa na serikali, kiliwakosoa maafisa wa usalama huko Malindi kwa “kupuuza wajibu na uzembe mkubwa”.
“Hawakushindwa tu kuwa makini katika kukusanya na kuchukua hatua za kijasusi ili kuzuia mauaji ya Shakahola lakini pia walishindwa bila sababu yoyote kuchukua hatua kulingana na ripoti za kuaminika,” mwenyekiti wa KNCHR Roseline odede alisema.