Mahakama nchini Pakistani imemhukumu mwanamke Mwislamu kifungo cha maisha jela baada ya kumpata na hatia ya kuchoma kurasa za kitabu kitakatifu cha Uislamu, mwendesha mashtaka alisema Ijumaa.
Chini ya sheria za kukufuru za Pakistan, yeyote atakayepatikana na hatia ya kukashifu dini au watu wa dini anaweza kuhukumiwa kifo,ingawa mamlaka bado hazijatoa hukumu ya kifo kwa kukufuru, shutuma tu zinaweza kuzua ghasia.
Mwendesha mashtaka wa serikali Mohazib Awais alisema mwanamke huyo, Aasiya Bibi, alikamatwa mwaka wa 2021 kwa tuhuma za kukufuru baada ya wakaazi kudai kuwa aliinajisi Quran kwa kuchoma kurasa zake.
Awais alisema hakimu alitangaza uamuzi huo Jumatano katika mji wa mashariki wa Lahore. Alisema Bibi, ambaye ana haki ya kukata rufaa, alikana shtaka hilo wakati wa kesi yake.
Mwanamke Mkristo aliye na jina kama hilo aliachiliwa kwa kosa la kukufuru mnamo 2019 baada ya kukaa miaka minane kwenye hukumu ya kifo nchini Pakistan.
Alihamia Kanada ili kuepuka vitisho vya kuuawa kutoka kwa watu wenye msimamo mkali wa Kiislamu baada ya kuachiliwa. Kesi ya Jumatano ilihusisha mwanamke tofauti.