Beki wa Valencia Christian Mosquera sasa ni mmoja wa wagombea wanaoongoza katika harakati za Atletico Madrid kutafuta beki wa kati kabla ya msimu ujao.
Atletico walikuwa wanamtaka Robin Le Normand wa Real Sociedad, lakini dili la mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania sasa linaweza kuwa ghali sana.
Mosquera, 19, amekuwa mchezaji muhimu wa Valencia msimu huu, akianza michezo 23 ya ligi, ambayo ilisababisha kuongezwa kwa mkataba wa moja kwa moja kwa mwaka mwingine, hadi 2026.
Hata hivyo kulingana na Marca, “uhusiano bora” kati ya Mkurugenzi Mtendaji wa Atleti Miguel Angel Gil na mmiliki wa Valencia Peter Lim unaweza kusaidia kufikia makubaliano.