Serikali ya wilaya ya Ilala imepiga marufuku michango mashuleni wanatozwa wanafunzi hali inayopelekea kurudishwa nyumbani kama hana fedha.
Kauli hiyo ameitoa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo baada ya kupokea kilio hicho cha wanawake wa jimbo la Segerea na kuwataka wampigie simu moja kwa moja kwa wanafunzi atakayerudishwa kwaajili ya michango.
“Wako baadhi ya walimu mashuleni wanawafanyisha watoto mitihani kila siku na kila wiki hapana, wala mtoto kuleta fedha kwa ajili ya chakula cha walimu na pesa za walinzi”
Akiwawakilisha wananchi hao Mbunge wa Jimbo la Segerea bonnah Kamoli amesema licha ya serikali kusema elimu ni bure bado kuna watoto wanaambiwa waende na fedha licha ya kuwa maisha kwasasa ni magumu.
“Hili swala la kuwaambia watoto waende na pesa shuleni wakati serikali mmesema watoto watasoma bure,sasa hivi maisha ni magumu na watu tuna watoto wengi haiwezikani kuwapa watoto wote hela tunaomba swala hilo liishe”.